Pale Mexime alipowaduwaza makocha wa kigeni na kutwaa tuzo
Na Saida Salum. Mlimani City
Kocha Mecky Mexime wa Kagera Sugar jana usiku alitwaa tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17.
Mexime ameiongoza Kagera Sugar na kufanikiwa kukamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa nyuma ya miamba Yanga SC waliotwaa ubingwa na Simba SC waliokamata nafasi ya pili.
Kutwaa kwa tuzo hiyo kwa mzalendo huyo, kumewafanya makocha wa kigeni wa timu za Simba na Yanga kushindwa kuambulia tuzo yoyote mbele yake, shukrani kwake Mecky Mexime ambaye aliwahi pia kuinoa Mtibwa Sugar ya Turiani mkoani Morogoro