BOCCO AMWAGA WINO MSIMBAZI
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Mshambuliaji hatari wa Klabu Bingwa Afrika mashariki na kati pamoja na kombe la Mapinduzi, Azam FC, John Raphael Bocco "Adebayor" amesaini mkataba wa miaka miwili katika timu ya Simba SC maarufu Wekundu wa Msimbazi.
Bocco amemwaga wino huo tayari kabisa kuitumikia Simba msimu ujao, nyota huyo akisifika mno akiwa katika kikosi cha Azam hasa kwa kuzitungua klabu kubwa na kongwe za Simba na Yanga.
Awali Yanga ilivumishwa kutaka kumsajili lakini baadaye dili la kujiunga nao likaishia njiani na Simba wakamalizana naye jana, Uongozi wa Azam FC haujawa tayari kuelezea kuondoka kwa mshambuliaji huyo ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo, Bocco alizaliwa mwaka 1989 jijini Dar es Salaam na amekuwa mmoja kati ya washambuliaji bora katika miaka ya hivi karibuni