Yanga watua kwa Gardiel Michael wa Azam
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, sasa vilabu kadhaa vimeanza kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao, Klabu bingwa ya soka nchini Yanga SC imeanza kubisha hodi kwa Azam FC na kutaka kumng' oa mlinzi wake wa pembeni Gadiel Michael.
Habari ambazo mtandao huu umezipata zinasema kuwa Yanga imeridhishwa na kiwango cha mlinzi huyo ambaye ameonyesha kiwango kikubwa msimu uliomalizika wa 2016/17 ingawa timu yake ya Azam kukamata nafasi ya nne.
Yanga wanataka kumchukua mlinzi huyo aliyemaliza mkataba na klabu hiyo na uhakika wa kutua Yanga unaonekana ni mkubwa, Kocha wa Yanga, Mzambia George Lwamdamina anataka kumtumia zaidi Gadiel kwani hakuridhishwa na Mwinyi Hajji ambaye amekuwa akipoozesha mashambulizi