Mecky Mexime akubali kutua Yanga

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Kocha Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Mecky Mexime wa Kagera Sugar amekubali kibarua cha kumsaidia kocha mkuu wa Ysnga Mzambia George Lwandamina.

Hivi karibuni kulikuwepo na taarifa kwamba Klabu ya Yanga inataka kumnasa Mexime ambaye aliiongoza vema timu ya Kagera Sugar na kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye ligi ya msimu huu uliomalizika.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ilisema kuwa kocha mkuu wa Yanga Mzambia George Lwandamina anamuhitaji Mexime ili awe msaidizi wake badala ya Juma Mwambusi.

Baada ya kuzisikia taarifa hizo, kocha Mecky Mexime amekubali kuwa kocha msaidizi wa Yanga akiamini ni timu kubwa na hapo ni sehemu sahihi kwake kujiendeleza kitaaluma, amewaomba Yanga wamfuate na kuingia naye kandarasi kwani hiyo ni kazi yake

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA