Jk amfuata Samata Ubelgiji
Rais mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Ally Samata anayekipiga katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji.
Kikwete yupo Ubelgiji kuhushuria mkutano wa kimataifa kuhusu Libya na ikumbukwe yeye ndiye msuluhishi wa mgogoro wa nchi hiyo iliyopo Afrika ya Kaskazini, (Pichani JK akiteta na Samata)