Mourinho aibebesha taji la Ulaya Man United
Tangu alipoondoka Mscotland Alex Ferguson katika kikosi cha Manchester United ya Uingereza, mambo yalikuwa hovyo kabisa alipotua Mscotland mwenzake David Moyes ambapo timu hiyo ilipoteza heshima yake.
Wengi walidhani ujio wa Luis Van Gaal raia wa Uholanzi mambo yangekuwa safi kwakuwa kocha huyo aliiongoza vema timu ya taifa ya Ujerumani kutwaa ubingwa wa kombe la Dunia michuano iliyofanyika nchini Brazil.
Ujio wa Mreno Jose Mourinho katika kikosi cha Manchester United pia wengi hawakutarajia maajabu ingawa kocha huyo amekuwa na maajabu mengi, tayari kocha huyo ameipa mataji matatu timu hiyo ila taji kubwa kabisa ni la Ulaya.
Jana usiku Man United imetwaa ubingwa wa kombe la Ueropa League baada ya kuilaza Ajax Amsterdam ya Uholanzi kwa mabao 2-0, hayo ni mafanikio makubwa kwa kocha huyo aliyewahi pia kuziongoza, Inter Milan, Chelsea na Real Madrid