BANDA ANAKWENDA AFRIKA KUSINI, AKIDUNDA KUSAINI YANGA

Na Ikram Khamees. Morogoro

Kiungo wa Simba anayemudu kucheza pia beki ya pembeni, Abdi Hassan Banda Jr, jana aliwaaga wapenzi na mashabiki wa Simba kwamba anaondoka zake katika timu hiyo kwenda kujaribu changamoto nyingine kwingineko.

Imefahamika kwamba kiungo huyo aliyewahi pia kuzichezea African Sports na Coastal Union zote za Tanga, anataka kwenda kujaribu bahati yake nchini Afrika Kusini lakini dili ikibuma anasaini Yanga miaka miwili.

Rafiki wa mchezaji huyo ambaye hakutaka kuandikwa jina lake amedai Banda anaenda Afrika Kusini ambapo alitakiwa na klabu moja ya huko lakini ishu hiyo ikibuma anasaini Yanga.

Banda aliwaaga mashabiki wa Simba jana kwenye mchezo wa fainali ya kombe la FA dhidi ya Mbao FC ambapo Simba ilishinda mabao 2-1 na kutwaa ubingwa, mchezo huo ulifanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA