Tshabalala awa mchezaji bora wa VPL
Na Saida Salum. Mlimani City
Tuzo ya mchezaji bora wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara ilinyakuliwa na mlinzi wa pembeni wa Simba SC Mohamed Hussein "Tshabalala" au Zimbwe Jr kama mwenyewe anavyojiita.
Tuzo hiyo ilitolewa usiku wa leo ambao pia ulihusisha tuzo kwa wachezaji wengine na vilabu, Yanga SC wenyewe waliondoka na tuzo tatu ikiwemo yao ya kutwaa ubingwa wa Bara na kuambulia kitita cha shilingi Mil 84.
Simon Msuva na Haruna Niyonzima waliing' arisha Yanga kwa kujizolea tuzo, Msuva alichukua tuzo ya ufungaji bora sambamba na Abdulrahman Musa wa Ruvu Shooting wakati Haruna Niyonzima yeye alishinda tuzo ya mchezaji bora wa kigeni.
Wengine waliobeba tuzo ni Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar alishinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wakati Mecky Mexime alishinda tuzo ya kocha bora