SIMBA MABINGWA WAPYA FA CUP 2016/17 WAIDUWAZA MBAO 2-1

Na Ikram Khamees. Dodoma

Mabao mawili yaliyofungwa na Muivory Coast, Fredrick Blagnon na Shiza Ramadhan Kichuya (Penalti) yametosha kabisa kuipa Simba ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Mchezo huo ulimalizika ndani ya dakika 120 baada ya kumaliza dakika 90 za mchezo timu hizo zikiwa 0-0, lakini katika dakika za nyongeza ikashuhudiwa magoli yote yakipatikana, Blagnon alikuwa wa kwanza kuifungia Simba bao la kuongoza kabla ya Mbao FC kusawazisha.

Shiza Kichuya zikiwa zimesalia dakika tatu mpira kumalizika akaipatia Simba bao la pili na la ushindi kwa mkwaju wa penalti uliotokana na mchezaji wa Mbao kuunawa mpira kwenye eneo la hatari, kwa matokeo hayo Simba wanakuwa mabingwa wapya na watashiriki michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika mwakani.

Pia Simba itaambulia shilingi Milioni 50 ambazo bingwa hujinyakulia, Hata hivyo wachezaji wa Mbao FC walimshutumu mwamuzi wa mchezo huo akidaiwa kutoa penalti kiupendeleo akiibeba Simba waziwazi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA