Sportpesa yazigonganisha Simba na Yanga
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa imetangaza kuanzisha michuano yake ya soka kwa ukanda huu wa Afrika mashariki itakayoshirikisha timu kutoka Tanzania Bara, Zanzibar na Kenya.
Michuano hiyo itafahamika kwa jina la Sportpesa Super Cup na itaanza Juni 5 mwaka huu, timu zote zinazodhaminiwa na kampuni hiyo ndizo zitakazoshiriki ambazo ni Yanga, Simba na Singida United kwa upande wa Bara.
Nyingine ni Nakuru All Star, Gor Mahia, Tusker FC na AFC Leopards zote za Kenya wakati Jang' ombe Boys ya Zanzibar nayo itashiriki michuano hiyo ambayo itafanyikia jijini Dar es Salaam, lengo na madhumuni ya kampuni hiyo ni kuendeleza soka la Afrika mashariki