AJIBU AWASHANGAA SINGIDA UNITED

Na Paskal Beatus. Dar es Salaam

Mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Ajibu Migomba anawashangaa Singida United kwa kitendo cha kumtangaza kwamba wanataka kumsajili wakati hawajawahi kumwita mezani.

Ajibu anashindwa kuwaelewa viongozi wa Singida United timu iliyopanda Ligi Kuu mwaka huu, Akizungumza Mambo Uwanjani, Ajibu amesema mkataba wake na Simba unamalizika mwezi ujao hivyo yuko tayari kusaini kokote.

Amedai Singida United inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Mholanzi Hans Van der Pluijm imeweka wazi mipango yake ya kumsajili Ajibu lakini bado haijafanya mazungumzo naye hivyo nyota huyo anaweza kuota mbawa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA