Sportpesa yamwondoa Manji Jangwani

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Kitendo cha Klabu Bingwa Tanzania Bara, Yanga SC kuingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa kimepelekea mwenyekiti wake Yusuf Mehbood Manji kujiuzuru wadhifa wake huo.

Manji ameandika barua ya kujizuru jana Mei 22 na amesema anawashukuru Wanayanga kwa mshikamano wao tangu alipoingia kwenye klabu hiyo miaka 16 iliyopita, Manji tangu alipochaguliwa kuiongoza klabu hiyo imetwaa ubingwa wa Bara misimu yote na kutengeneza kikosi bora ambacho kiliwahi kuingia hatua ya makundi kombe la Shirikisho.

Inasemekana kiongozi huyo ameamua kujiuzuru kwa sababu ya mkataba wa Sportpesa ambao utazifanya jezi za Yanga kuitangaza kampuni hiyo badala ya Quality Group, uamuzi huo wa Yanga kuingia mkataba na kampuni hiyo halikuwa pendekezo lake isipokuwa ni wazo la watu wachache ambao walitaka kuingia ndani ya Yanga hasa baada ya yeye kuyumba alipokuwa na matatizo na serikali

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA