Yanga bingwa 2016/17
Na Paskal Beatus. Mwanza
Yanga SC ya Dar es Salaam leo imefanikiwa kuweka rekodi ya miaka kadhaa baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara licha ya kufungwa bao 1-0 na Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Yanga imetwaa ubingwa huo baada ya kushuka uwanjani mara 30 ikifikisha pointi 62 ambazo zimefikiwa na mahasimu wao Simba SC waliopata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Baadhi ya matokeo ya mechi nyingine ni Kagera Sugar 1 Azam Fc 0, Mtibwa Sugar 3 Toto Africans 1, matokeo mengine tutaendelea kuwajuza lakini Toto Africans, African Lyon na JKT Ruvu zimeshuka daraja