Atupele Green rasmi Singida United
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Kagera Sugar na JKT Ruvu, Atupele Green Jackson amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Singida United iliyopanda Ligi Kuu.
Atupele ambaye timu yake ya JKT Ruvu imeshuka daraja, ameamua kujiunga na Singida iliyokuwa ikimuhitaji, Singida United imekuwa ikijiimarisha kwenye usajili na tayari imeshawanasa wachezaji sita mpaka sasa wenye uzoefu.
Kutua kwa mshambuliaji huyo ambaye mwaka jana aliibuka mfungaji bora kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup maarufu kombe la FA, ila mwaka huu tuzo hiyo amenyang' anywa na Mzambia Obrey Chirwa wa Yanga ambaye ndiye mfungaji bora.
Wakati huo huo beki wa Mbao Fc ya Mwanza, Asante Kwasi ameigomea ofa ya Singida United na kuweka wazi mipango yake ya kutaka kujiunga na Azam FC, Asante Kwasi kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumalizika kwa mkataba wake kwenye timu hiyo ya Mbao