Serengeti Boys waanza kwa sare Gabon
Na Ikram Khamees. Libreville
Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania maarufu Serengeti Boys jioni ya leo imewalazimisha sare ya 0-0 mabingwa watetezi wa michuano hiyo Mali katika mchezo wa kwanza kundi B Uwanja wa I' Amitie Sino jijini Libreville.
Mchezo huo ulikuwa wa upande mmoja na Mali walionekana kuutawala muda wote lakini shukrani pekee ziwaendee mabeki wa Serengeti Boys ambao walifanya kazi ya ziada na kulinda muda wote.
Wachezaji wa Mali ambao wana uzoefu mkubwa na michuano hiyo walishindwa kuupita ukuta wa Serengeti na kumaliza mchezo kwa sare na wakiambulia pointi moja