Mbaraka Yusuf Abeid mchezaji bora chipukizi VPL
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Mshambuliaji chipukizi wa Kagera Sugar ya Misenyi Bukoba mkoani Kagera, Mbaraka Yusuf Abeid usiku wa jana katika ukumbi wa Mlimani City Hall jijini Dar es Salaam alishinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa msimu uliomalizika wa 2016/17 ambapo timu yake imemaliza katika nafasi ya tatu.
Mbaraka alikuwa mmoja kati ya washambuliaji chipukizi waliofanya vizuri kwenye ligi hiyo kiasi kwamba aliweza kuzichachafya Simba na Yanga, Mbaraka alifunga kwenye mechi zote mbili alizokutana na Simba pamoja na Yanga.
Pia chipukizi huyo aliitwa timu ya taifa, Taifa Stars na aliweza kufunga bao muhimu ambalo liliipa ushindi Stars wa mabao 2-1 dhidi ya Burundi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam