Wanaowania tuzo ya mchezaji bora VPL hawa hapa

Wachezaji watano wameteuliwa (nominees) kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2016/2017.

Walioteuliwa kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho ni Aishi Manula (Azam FC), Haruna Niyonzima (Yanga), Mohamed Hussein (Simba), Shiza Kichuya (Simba) na Simon Msuva (Yanga).

Majina hayo yatapigiwa kura na makocha, makocha wasaidizi na manahodha wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na wahariri wa michezo kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Wahusika watatumiwa fomu maalum za kupiga kura kwenye email za klabu zao na vyombo husika vya habari. Mwisho wa kupiga kura ni saa 6 usiku ya Jumanne, Mei 23 mwaka huu.

Hafla ya kutoa tuzo hiyo ambayo inaratibiwa na Kamati ya Ushauri ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika Mei 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA