Sanchez, Ramsey waing' arisha Arsenal England
Magoli mawili yaliyofungwa na Alexis Sanchez na Aoron Ramsey yalitosha kabisa kuipa ushindi Arsenal wa mabao 2-1 dhidi ya Chelsea katika mchezo wa fainali ya kombe la FA Uwanja wa Wembley London.
Sanchez alitangulia kufunga bao la kwanza kabla ya Diego Costa kuisawazishia Arsenal kwa bao maridadi lililotokana na juhudi zake binafsi, Lakini Aoron Ramsey alikatisha matumaini ya Chelsea kutaka kuongeza kikombe cha pili msimu huu baada ya kufunga bao la ushindi.
Bao hilo lilifungwa dakika ya 79 na liliwapa ubingwa Arsenal ambao msimu huu wamemaliza katika nafasi ya tano EPL, Mkufunzi wa Arsenal, Arsenel Wenger alifurahia ubingwa huo wa FA na kusema msimu huu alikutana na changamoto nyingi na anashukuru vijana wake hawakumwangusha