Hivi ndivyo beki wa zamani wa Simba alivyoagana na ukapela
Beki wa zamani wa Simba SC, Salum Mpakala "Distance" hivi karibuni alifunga ndoa na kuachana na ukapela, Mpakala aliwahi kuichezea Simba miaka ya 2003 hadi 2004 wakati Simba ikitikisa.
Baada ya kuachana na Simba, nafasi yake akasajiliwa Salum Kanoni, Mpakala alisajiliwa na Simba akitokea Vijana ya Ilala sambamba na kipa Haji Macharazi.
Baada ya kuachana na Simba nyota huyo alienda Namibia sambamba na Madata Lubigisa kucheza soka la kulipwa kisha akatimkia Sweden ambako alikaa mpaka mwaka jana aliporejea Dar es Salaam na kuendelea na maisha mengine nje ya soka