Infatinho alipoikatia umeme Simba SC
Jana kulizuka taarifa mitandaoni kwamba Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani ameitumia salamu za pongezi Klabu Bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga SC kupitia kwa Rais wa Shirikisho la kandanda Tanzania, (TFF) Jamal Malinzi.
Taarifa hizo zilionekana kupuuzwa na mahasimu wa Yanga, Simba SC ambao walisikika wakisema kwamba zimetengenezwa na watu wa Yanga, wanadai FIFA haiwezi kuwatumia salamu Yanga kwakuwa Simba imekata rufaa ikitaka ipewe pointi za chee dhidi ya Kagera Sugar.
Lakini kwa mujibu wa TFF taarifa hizo za salamu za Rais wa FIFA, Gian Infantinho ni kweli ameitumia salamu TFF kwa kukamilisha vema Ligi Kuu ya soka ya Tanzania na kumpata bingwa mpya ambaye ni Yanga SC