Yanga nao waingia mkataba na Sportpesa miaka mitano
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Mabingwa wa soka nchini Yanga SC wameingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya michezo ya bahati nasibu ya Sportpesa wenye thamani ya shilingi Bilioni 5.173 za Kitanzania.
Mkataba huo kati ya Yanga na Sportpesa utaifanya Yanga ichukue shilingi Milioni 950 kwa mwaka, hii itawafanya wawalipe mishahara wachezaji wake bila matatizo yoyote.
Ujio wa Sportpesa umeleta faraja kwa vilabu vya Simba na Yanga ambavyo sasa vitaanza kujiendesha vyenyewe kuliko hapo nyuma ambapo viliendesha kwa fedha za watu