Msuva na Mussa kulamba zawadi ya mfungaji bora VPL
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF), Jamal Emili Malinzi amesema tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara maarufu VPL itakwenda kwa Simon Msuva wa Yanga na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting.
Wachezaji hao wote wawili wamefunga mabao 14 kila mmoja na kuwafanya wagawane zawadi ya mfungaji bora inayotolewa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya simu Vodacom.
Tuzo zinatarajiwa kutolewa Mei 24 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam,