Everton kutua Dar es Salaam Juni

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Timu ya Everton ya Uingereza itawasili jijini Dar es Salaam mwezi ujao na itacheza mechi yake ya kirafiki katika Uwanja wa Taifa, vigogo hao wa Uingereza wataletwa nchini na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa.

Kwa mujibu wa tovuti ya Everton imesema kwamba, timu hiyo itatua Dar es Salaam kwa mwaliko wa Sportpesa na watacheza mchezo mmoja wa kirafiki na timu itakayochukua ubingwa wa michuano ya Sportpesa Super Cup inayotarajia kuanza Juni 5 mwaka huu.

Bingwa wa michuano hiyo mbali na kujinyakulia kikombe na shilingi Milioni 60, pia atapata fursa ya kucheza na Everton moja kati ya timu zinazosumbua Uingereza

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA