Haruna Niyonzima alivyowabwaga wageni wenzake
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Haruna Hakizimana Fadhili Niyonzima (Pichani) raia wa Rwanda, jana usiku katika ukumbi wa Mlimani City alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2016/17.
Niyonzima alishinda tuzo hiyo kwa wachezaji wa kigeni ambapo ameweza kuwaangusha nyota wenzake wanaotoka nje, Niyonzima alidhihirisha hilo pale alipojitokeza kuisaidia Klabu yake kutwaa ubingwa wa Bara kwa msimu huu.
Mchango wake ulikuwa ukionekana uwanjani ambapo anapokosekana pengo lake lilijionyesha dhahili na pale anapoingia makali yake huonekana, Niyonzima ni nahodha msaidizi wa Yanga pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda, Amavubi Stars