Stars yaangukia mikononi mwa Angola, Cosafa Cup

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepangwa kundi A katika michuano ya mataifa ya Afrika yaliyo ukanda wa kusini maarufu Cosafa Cup ambayo yanatarajia kuanza mwezi ujao.

Kwa mujibu wa waandaaji wa michuano hiyo, Cosafa inaonyesha Stars imeangukia kundi A litakalokuwa na timu nne wakati kundi B nalo lina timu nne, hii ni mara ya pili kwa Stars kushiriki michuano hiyo yenye msisimko mkubwa tofauti na michuano ya Chalenji inayoshirikisha timu za ukanda wa Afrika mashariki.

Katika michuano hiyo itakayofanyika nchini Afrika Kusini, Stars imepangwa na Angola, Malawi na Mauritius mataifa mengine manne yatakayokuwa kundi B ni Msumbiji, Zimbabwe na Shelisheli

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA