Masikini Mkude! Atemwa Stars
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Nahodha msaidizi wa timu ya taifa, Taifa Stars, Jonas Gerald Mkude ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa kitakachoondoka kesho kuelekea Cairo Misri kwa ziara ya wiki moja kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Lesotho Juni 10.
Akizungumza leo, Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Alfred Lucas amesema Mkude ameenguliwa kwenye kikosi hicho kutokana na ushauri wa madaktari hasa baada ya kupata ajali.
Mkude alipata ajali jana baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Dodoma kupinduka maeneo ya Dumila mkoani Morogoro na kusababisha majeruhi wanne akiwemo yeye huku mwenzao mmoja, Shose Fideris kuaga dunia.
Mkude aliiongoza Simba kutwaa ubingwa wa kombe la FA baada ya kuilaza Mbao FC mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma juzi, na wakiwa njiani na gari lao aina ya Range Cluiser V8 lilipasuka tairi na kuhama njia