JONAS MKUDE ANUSURIKA KIFO DUMILA
Na Ikram Khamees. Morogoro
Nahodha wa Mabingwa wa kombe la FA, Simba SC, Jonas Gerald Mkude amenusurika kifo katika ajali mbaya ya gari iliyotokea maeneo ya Dumila mkoani Morogoro.
Mkude na wenzake watano akiwemo mwanachama maarufu wa Klabu hiyo ambaye ndiye mmiliki wa gari hilo Ahmed Kassim kwa jina maarufu Rais wa Kibamba waliumia vibaya baada ya gari lao Range Cluiser V8 kuhama njia na kutokomea porini baada ya tairi la mbele kupasuka.
Mashabiki wa Simba waliokuwa wakitokea mkoani Dodoma kuangalia fainali ya kombe la FA ambapo ilichezwa jana na timu ya Simba kutwaa ubingwa baada ya kuilaza Mbao FC ya Mwanza kwa mabao 2-1 walijitokeza kuwasaidia majeruhi wa ajali hiyo akiwemo Mkude.
Hata hivyo hali ya afya ya Mkude inaimarika na wala hajaumia sana anaendelea vizuri huku inadaiwa katika ajali hiyo kulikuwemo na abiria mmoja wa kike aliyefahamika kwa jina la Shose mkazi wa Dar es Salaam amefariki dunia kwenye ajali hiyo na mwili wake umehifadhiwa hospitalini na utasafirishwa Dar es Salaam