Singida United yaibomoa Yanga

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Timu ya Singida United ya mkoani Singida imeendelea kuimarisha kikosi chake hasa baada ya kubisha hodi kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC na kumnasa kipa wake Ally Mustapha "Barthez".

Taarifa zenye uhakika ambazo Mambo Uwanjani haizitilii shaka zinasema kuwa Singida Unied iko mbioni kumpa mkataba wa miaka miwili kipa huyo ambaye amekuwa na bahati mbaya katika kikosi cha Yanga kwani hakutumika karibu msimu mzima.

Tayari Singida United imeshamnasa kiungo wa Mbeya City, Kenny Ally ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili, timu hiyo inanolewa na kocha wa zamani wa Yanga SC, Mholanzi Hans Van der Pluijm na msimu ujao itashiriki Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA