Malinzi amlilia Shose wa Simba

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu hapa nchini TFF, Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Klabu ya Simba kufuatia msiba wa mpenzi na shabiki wake Shose Fideris.

Shose alifariki dunia jana katika ajali ya gari iliyotokea Dumila mkoani Morogoro, gari aina ya Range Cluiser iliyokuwa ikiendeshwa na Ahmed Kassim au Rais wa Kibamba kama anavyofahamika kupasuka tairi na kutokomea porini.

Ndani ya gari hilo pia alikuwemo nahodha wa Simba Jonas Mkude ambaye aliumia sambamba na dereva na watu wengine wawili, Mkude na wenzake walitokea Dodoma ambako juzi Simba ilicheza fainali na Mbao Fc na kushinda mabao 2-1 na kutwaa ubingwa wa FA Cup kwenye uwanja wa Jamhuri.

Wakiwa njiani ndipo ajali hiyo ilipotokea na kusababisha kifo cha shabiki huyo kindakindaki wa Simba, Malinzi amewapa majeruhi wa ajali hiyo na akisikitishwa na kifo cha shabiki huyo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA