Shabiki kindakindaki wa Simba aliyefariki ajalini Dumila
Na Mwandishi Wetu. Morogoro
Jumapili ya Mei 28 imetokea ajali mbaya ya gari maeneo ya Dumila mkoani Morogoro ambapo gari aina ya Range Cluiser V8 inayomilikiwa na shabiki mwingine wa Simba Ahmed Kassim "Rais wa Kibamba" kupata ajali mbaya na kusababisha kifo cha mwanadada Shose Fideris.
Kwa mujibu wa mashabiki wa Simba waliojitokeza kusaidia kuokoa majeruhi akiwemo nahodha na kiungo wa Simba, Jonas Gerald Mkude na mmiliki wa gari na abiria wengine, Shose alifariki papo hapo, ajali hiyo imetokea baada ya gari hilo kupasuka tairi la mbele na kuingia porini.
Mipango ya kuuleta mwili wa shabiki huyo kindakindaki wa Simba ambayo jana ilitwaa ubingwa wa kombe la FA kwa kuilaza Mbao FC katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Simba ilishinda mabao 2-1