Ni fainali ya maajabu Simba na Mbao FC
Na Ikram Khamees. Dodoma
Uwanja wa Jamhuri Stadium mjini Dodoma ambako ni makao makuu ya serikali itapigwa fainali ya aina yake Jumamosi ya Mei 28 kati ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC na Mbao FC vijana wanaocheza kandanda la hali ya juu wanaotokea jijini Mwanza.
Maajabu ya fainali hiyo ni kwamba endapo Mbao FC itashinda mchezo huo basi itakuwa timu ya kwanza kutoka mikoani kuwakilisha taifa katika michuano ya kimataifa mwakani, Mbao itashiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Mchezo huo wa fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFA) maarufu kombe la FA utakuwa na maajabu mengi ikiwemo Simba kupata tiketi ya kuwakilisha taifa kwa mara ya kwanza baada ya kukosa kwa miaka minne mfululizo.
Timu zote mbili zina vikosi imara na yeyote anaweza kuchomoza na ushindi, Mbao FC mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoka kuitoa nishai Yanga baada ya kuilaza bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu Bara uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, pia utakuwa ni mchezo wa kisasi kwani Mbao wana kumbukumbu ya kufungwa na Simba mabao 3-2