Msuva kuikosa Toto leo
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Winga wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC, Simon Msuva atakosekana katika mchezo wa leo dhidi ya Toto Africans Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Msuva anaukosa mchezo huo muhimu ambao unaweza kumpa ama kumnyima tuzo ya ufungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Msuva anaongoza kwa mabao akiwa amefunga mabao 14 akifuatiwa na Abdulrahaman Mussa.
Msuva aliumia eneo la usoni wakati akifunga bao wakati Yanga ikiilaza Mbeya City mabao 2-1, Msuva alifunga bao kwa jitihada zake binafsi na kwa bahati mbaya aliumizwa katika harakati za kufunga.
Endapo Yanga itashinda katika mchezo wa leo itakuwa imefikisha pointi 68 na itakuwa tayari imeshajihakikishia ubingwa wa Bara