Shose wa Simba kuagwa Alhamisi
Na Paskal Beatus. Dar es Salaam
Yule shabiki wa Klabu ya Simba Shose Fideris aliyefariki katika ajali ya gari iliyotokea Dumila mkoani Morogoro ambapo ndani yake alikuwemo nahodha wa Simba Jonas Mkude ataagwa Alhamisi ijayo.
Shabiki huyo ataagwa Alhamisi kuanzia saa 5:00,asubuhi katika hospitali ya Mwananyamala kisha saa 7:00 mchana katika kanisa katoliki Magomeni, na atasafirishwa mkoani Kilimanjaro na kuzikwa Ijumaa, marehemu Shose alifariki wakati gari alilopanda akitokea Dodoma kutazama mchezo wa fainali kati ya Simba SC ya Dar es Salaam na Mbao FC.
Katika mchezo huo Simba ilishinda mabao 2-1 na kutwaa kombe la FA, Wakiwa njiani kurejea Dar es Salaam wakisafiri na gari aina ya Range Cluiser V8 iliyokuwa ikiendeshwa na Ahmed Kassim "Rais wa Kibamba" ambaye ndiye mmiliki, lilipasuka tairi la mbele kuingia porini
Kwa niaba ya Mtendaji mkuu wa Mambo Uwanjani Publishers inatoa salamu za pole kwa familia ya Shose na wapenzi na mashabiki wa Simba SC