CAF YAWAPA YANGA WAANGOLA
Na Exipedito Mataruma, CAIRO
SHIRIKISHO la kandanda barani Afrika CAF limeipangia klabu ya Yanga ya Tanzania kucheza na Segrada Esperance ya Angola (Pichani) mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika.
Yanga na Esperance zimeangukia kombe la Shirikisho baada ya kuondoshwa kwenye ligi ya mabingwa Afrika, Yanga ilifungwa mabao 2-1 jana usiku na Al Ahly ya Misri uwanja wa Borg Al Arab mjini Alexandria.
Mechi za mchujo kombe la Shirikisho kuelekea kwenye makundi zinataraji kuchezwa kati Mei 6-7 na marudiano kuchezwa kati Mei 17-18, hiyo ni nafasi nyingine kwa Yanga kuandika rekodi kwani ikivuka hatua hiyo itaingia Robo fainali