KOCHA AZAM AIGWAYA YANGA FAINALI YA FA CUP
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM
KOCHA mkuu wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati Muingereza Stewart Hall amesema Yanga Sc haikustahili kucheza fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup kwani imebebwa na TFF.
Akizungumza na vyombo vya habari, Hall amesema aliutazama mchezo wa Nusu fainali kati ya Yanga na Coastal Union uliofanyika uwanja wa Mkwakwani Tanga ambapo Yanga ilishinda mabao 2-1 na mchezo huo ukavunjika kutokana na vurugu.
Muingereza huyo aliyeiwezesha Azam kutwaa kombe la Kagame amedai Yanga ilibebwa na waamuzi kwani magoli yote iliyofunga hayakuwa halali, Stewart amesema kwamba upendeleo huu wa waamuzi hauvumiliki.
TFF chini ya kamati yake ya mashindano iliamua kuipa ushindi Yanga hasa baada ya kujiridhisha Coastal walifanya vurugu kupitia kwa mashabiki wake na pia waamuzi waliboronga kwani iliwaadhibu.
Kwa kauli hiyo ni sawa kama anaigwaya Yanga kwani atakutana nayo kwenye mchezo wa fainali itakayopigwa Mei mwaka huu