AZAM TV KURUSHA LIVE MECHI YA AZAM NA ESPERANCE SAA 3 USIKU
Na Salum Fikiri Jr, TUNISIA
MPAMBANO unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka nchini Tanzania kati ya Azam na Esperance sasa utarushwa live na Azam Tv.
Mpaka sasa ni asilimia 100 kuwa mechi kati ya Azam FC na Esperance ya Tunisia itakayofanyika leo saa 3.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, itarushwa moja kwa moja kupitia Kingamuzi cha Azam TV (Azam TWO).
Hivyo mashabiki wa Azam FC pamoja na Watanzania kwa ujumla kaeni mkao wa kula kutazama mpambano huo, kama ulikuwa ujalipia Kingamuzi cha Azam TV, tafadhali lipia haraka ili uweze kushuhudia mchezo huo.
Kama hiyo haitoshi, ukurasa huu utakuwa ukikupa matokeo 'live' kwa kila kinachojiri ndani ya Uwanja wa Olympique de Rades.