VIPORO VYA 'WAKUDA', YANGA NA AZAM LEO DAR
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM
YANGA SC na Azam Fc jioni ya leo wote kwa pamoja wanataraji kushuka dimbani kukamilisha viporo vyao, katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, mabingwa wa bara Yanga Sc wataialika Mgambo JKT ya Tanga.
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo ili izidi kujiweka katika mazingira mazuri, mabingwa hao wa bara wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 59 na mechi 24 wakifuatiwa na Simba yenye pointi 57 mechi 25.
Mgambo JKT vijana wa Kabuku wilayani Handeni mkoani Tanga nao hawatakubali kupoteza mchezo huo kwani wapo sehemu mbaya ya kushuka daraja.
Mtanange mwingine upo uwanja wa Azam Complex ambapo wenyeji "Wauza Ice Cream wa Bakhressa" Azam Fc wanawaalika "Wapiganaji wa vita ya Majimaji" kutoka Songea, Azam inahitaji ushindi ili iweze kukwea hadi nafasi ya pili ikiwashusha Simba.
Azam hadi sasa ina pointi 55 mechi 24 ikishinda mchezo huo itafikisha pointi 58 na kuiacha Simba kwa tofauti ya pointi moja Waikato Jumapili miamba hiyo Azam na Simba watakutana uwanja wa Taifa