MWILI WA PAPA WEMBA WAWASILI DRC
Na Mwandishi Wetu, DRC
MWILI wa aliyekuwa mwanamuziki gwiji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Papa Wemba aliyefariki jukwaani akitumbuiza mjini Abidjan umewasili leo na kupokewa uwanja wa ndege wa Kinshasa.
Mamia ya waombolezaji walijitokeza kwa wingi kushuhudia jeneza lililobeba mwili wa muasisi huyo wa miondoko ya kizazi kipya ya Soukous, Papa Wemba alifariki jukwaani Aprili 14, 2016 akiwa kwenye shoo zake za muziki.
Mke wa marehemu aliyeambatana na wasaidizi wake aliudhuria uwanja wa ndege wa Kinshasa kushuhudia mwili wa mumewe, baadhi ya watu waliofurika uwanjani hapo walionekana kuwa na hisia na kutokwa na machozi hasa pale jeneza lake lilipotelemshwa kutoka kwenye ndege.
Rais wa DRC Joaeph Kabila alituma ndege nchini Ivory Coast kufuata mwili wa gwiji huyo wa muziki aliyeitangaza nchi hiyo nje ya mipaka, Papa Wemba atazikwa hivi karibuni