YANGA WATAKIWA KUFANYA UCHAGUZI JUNI 5
Na Mwandishi Wetu DAR EA SALAAM
SHIRIKISHO la soka nchini TFF limeitaka klabu ya Yanga kuitisha uchaguzi wake ifikapo Juni 5 kulingana na agizo lilikotolewa na BMT na wizara.
Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi TFF, Aloyce Komba amesema mchakato mzima wa uchaguzi wa Yanga utakuwa ndani ya siku 33.
Komba ambaye pia ni Wakili, amesema mchakato rasmi wa uchaguzi wa Yanga utaanza Mei 3, 2016, Komba amesema jukumu lao TFF kusimamia na kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika hali ya demokrasia.
Wakili Komba ameongeza kuwa kamati yake itatangaza mchakato mzima wa uchaguzi huo wa Yanga na kubandika tangazo kwenye mbao za matangazo na kutangaza nafasi zitakazogombaniwa.
Mei 4-9, 2016 kuchukua fomuza wagombea na mwisho wa kurudisha kwa wagombea, Mei 10, 2016 kamati ya uchaguzi TFF itakaa kikao cha mchujo wa awali wa wagombea na kuandika barua za kuwajulisha wagombea juu ya mchujo huo wa awali.
Mei 11, 2016 kamati ya uchaguzi ya TFF itachapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo orodha ya awali ya wagombea, Mei 12-13_ 2016 kipindi cha kupokea na kuweka pingamizi kwa wagombea wote.
Mei 14-15, 2016 kamati ya uchaguzi TFF itapitia pingamizi zote na kufanya usajili wa wagombea, Mei 16, 2016 kamati ya uchaguzi TFF itatangaza na kubandika kwenye mbao za matangazo matokeo ya awali ya usahili.
Mei 17, 2016 Sekretalieti kuwasilisha masuala ya kimaadili kwenye kamati ya maadili ya TFF, Mei 18-19, 2016 kamati ya maadili ya TFF itappkea na kusikiliza na kutolea maamuzi ya kamati maadili.
Ratiba kamili ya uchaguzi inaonyesha kuwa Mei 20, 2016 kamati ya maadili itatangaza maamuzi ya masuala ya kimaadili, Mei 21-22 kipindi cha kukata rufaa, Mei 23, kamati ya maadili TFF itasikiliza rufaa.
Mei 24, kamati ya rufaa na maadili itatoa maamuzi ya rufaa, Mei 25 na 26 kipindi cha kukata rufaa kwa kamati ya uchaguzi dhidi ya kamati ya TFF, Mei 27-28 muda wa kusikiliza rufaa na Mei 29 kamati ya uchaguzi itatangaza maamuzi ya rufaa.
Mei 30 kamati ya uchaguzi itachapisha orodha ya majina ya wagombea na kubandikwa kwenye mbao za matangazo, Mei 31 na Juni 4, kipindi cha kampeni kwa wagombea na Juni 5 ni siku ya uchaguzi mkuu wa klabu ya Yanga