KWA WAPENZI WA FILAMU, MSIKOSE MZIGO MPYA UNAKUJA
Na Saida Salum, DAR ES SALAAM
SOKO la filamu nchini linazidi kuongezeka kufuatia wasanii mbalimbali nchini kuzidi kutengeneza filamu zenye ubora wa kipekee na wa hali ya juu.
'The Dead Samson' ni moja kati ya filamu inayosubiriwa kutoka hivi karibuni na tayari imeshaanza kuwa gumzo ambayo ndani yake yupo mwanadada anayeibukia kwa sasa kwenye tasnia hiyo Rachel Bithulo 'Recho'.
Mwanadada anayetokea Mwanza, amezidi kujipatia umaarufu kutokana na kazi zake na kufanya vizuri, Ector huyo wa kike pia ni Video Queen wa bongofleva na wimbo uliompa saluti ni ule wa PNC uitwao 'Yule yule', ambao alikubalika vilivyo na kuwavutia wengi.
Mbali na kutamba kwenye filamu hiyo, Recho pia amewahi kutamba kwenye filamu ya 'Craritha' ambayo ilimtangaza kama msanii wa kike anayefanya vizuri, msanii huyo alipata bahati kuingia kwenye tuzo za Nyambago Award 2016 lakini hakubahatika kupata tuzo na hasa mchakato wenyewe kudaiwa kuwa na upendeleo kwa wasanii wa kanda ya ziwa