YANGA WAWASILI MWANZA KIBABE
Na Paskal Beatus, MWANZA
YANGA ya Dar es Salaam imewasili asubuhi ya leo hapa jijini Mwanza ikitokea Dar es Salaam ambako jana jioni iliichapa Mgambo JKT ya Tanga mabao 2-1 uwanja wa Taifa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Kikosi cha Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo wametua na wachezaji wao wote mapema na kulakiwa na mashabiki wake waliojitokeza uwanja wa ndege.
Jumamosi ijayo Yanga itakuwa mgeni wa Toto Africans "Wanakishamapanda" uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa, tayari Yanga inaongoza ligi ikiwa kibindoni na pointi 62 mechi 25 na inahitaji pointi tatu muhimu ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa bara.
Vijana wa Toto nao wanataka kudhihirisha kuwa hawakubahatisha kuwafunga Simba Sc bao 1-0 uwanja wa Taifa Dar es Salaam hivyo kulufabya pambano hilo kuwa kali na la kuvutia