PAPA WEMBA AFARIKI DUNIA IVORY COAST
Na Mwandishi Wetu, KIMATAIFA
MWANAMUZIKI maarufu barani Afrika Papa Wemba raia wa DRC amefariki dunia ghafla mjini Abidjan akiwa anafanya maonyesho yake ya kimuziki na ghafla alipatwa na maradhi na kupelekea kifo chake.
Mwanamuziki huyo aliyejipatia umaarufu mkubwa kwa miondoko yake ya muziki wa Kikongo huku akipata mialiko mbalimbali katika nchi za Ufaransa na Ubelgiji.
Marehemu pia atakumbukwa na wapenzi wa muziki nchini Tanzania nao wanamkumbuka vilivyo kwani aliwahi kuitembelea nchi hiyo na kufanya maonyesho kadhaa.
Papa Wemba alizaliwa Juni 14, 1949 katika mji wa Lubefu, Belgian DRC Congo na alipata kuhudumu katika bendi za Zaiko Langa Langa na Viva la Musica, marehemu Papa Wemba ndio jina lililovuma sana lakini jina halisi ni Jules Shungu Pene Wembadio Kikumba