FARID MUSSA ATIMKIA HISPANIA KUJARIBU BAHATI
Na Salum Fikiri Jr, TUNISIA
Farid huyooo Malaga, Las Palmas
--------------------------------------------------------
WINGA chipukizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Farid Mussa, kesho Ijumaa anatarajia kuondoka nchini hapa Tunisia kuelekea Hispania kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
Farid atakuwa huko kwa takribani mwezi mmoja na atafanya majaribio katika timu za Malaga na Las Palmas zinazoshiriki Ligi Kuu ya nchini humu na atarejea jijini Dara es Salaam May 19 mwaka huu msimu wa ligi ukiwa umeisha.
Farid amekuwa katika kiwango cha juu akiwa na klabu yake ya Azam na akawa miongoni mwa wachezaji walioifungia magoli timu hiyo ya bilionea Said Salim Awadh Bakhressa na familia yake ilipoiduwaza 2-1 Esperance ya Tunisia katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam