ESPERANCE YAIFURUSHA AZAM KOMBE LA SHIRIKISHO
Na Salum Fikiri Jr, TUNISIA
AZAM FC imeaga michuano ya kombe la Shirikisho la soka barani Afrika baada ya kufungwa mabao 3-0 na wenyeji Esperance katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 bora usiku wa leo Uwanja wa Olympique de Rades mjini Tunis.
Matokeo hayo yanaifanya Azam Fc inayomilikiwa na bilionea Said Salim Bakhressa na familia yake itolewe kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya awali kushinda 2-1 Dar es Salaam.
Ikicheza mchezo wa kujihami kwa kutumia viubgo watano na mshambuliaji mmoja tu, Nahodha John Raphael Bocco, Azam ilifanikiwa kuwabana vizuri wenyeji dakika 45 za kwanza na kumaliza bila kuruhusu bao.
Timu hiyo ya kocha Muingereza Stewart Hall ilikuwa ikifanya mashambulizi ya kushitukiza kwa kumpelekea mipira mirefu Bocco, ambaye hata hivyo alidhibitiwa, ukuta wa Azam ukifanya kazi ya ziada ya kuzuia mashambulizi ya Esperance muda mwingi wa kipindi hicho huku kipa wake Aishi Manula akiokoa michomo zaidi ya minne ya hatari langoni mwake.
Hata hivyo, bao la mapema kipindi cha pili walilopata Esperance lilitibua mipango ya Azam na kuchanganyajiwa.
Bao hilo lilifungwa na Saad Bguir dakika ya 47 kwa shuti la mpira wa adhabu umbali wa mita 19, baada ya Fakhreddine Ben Youssef kuangushwa na David Mwantika nje kidogo ya boksi.
Baada ya hilo, Azam Fc walibadilisha mfumo na wao kuanza kushambulia moja kwa moja na hapo ndipo mchezo ukaanza kuwa wa pande zote.
Hata hivyo kufunguka kwa Azam kuiipa nafasi Esperance na kufanikisha mipango yake na kuongeza mabao mengine mawili yaliyopatikana dakika ya 63 na 80 yakifungwa na Haithem Jouini na na Fakhreddine Ben Youssef tena.
Pengo la kuwakosa wachezaji wake wanne Shomari Kapombe, Kipre Tchetche, Paschal Wawa na Jean Bapstita Mugilaneza kuliokana dhahili kuiathili Azam kwani hawakuweza kulitia msukosuko tena lango la Esperance