STARS KUJIPIMA NA HARAMBEE STARS MEI 29
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM
TIMU ya taifa ya Tanzanja Taifa Stars inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars ifikapo Mei 29 mjini Nairobi Kenya.
Mchezo huo unatosha kuzipa mazoezi tosha timu zote mbili za ukandaa huu wa Afrika mashariki na kati ambapo Juni mwaka huu zitakuwa na vibarua vya kufuzu fainali za mataifa Afrika.
Stars inayonolewa na mzalendo Charles Boniface Mkwassa itakuwa na mtihani mgumu wa kuipiku Misri "Farao" katika kuipata tiketi ya kufaulu kwenye kundi lake.
Hadi sasa Stars na Misri ndizo zenye nafasi ya kufuzu fainali za AFCON kutokana na mazingira yenyewe, Stars ina pointi moja iliyopata dhidi ya Nigeria ambayo imeshatolewa tayari, Misri wanapointi 5 na wamesaliwa na mechi moja, wakati Stars imebakiza mechi mbili na ikishinda zote itafikisha pointi 7 na moja kwa moja itafuzu kwenda Gabon mwakani.
Misri na Tanzania zitaumana Juni mwaka huu jijini Dar es Salaam, imepita miaka kadhaa Stars na Harambee hawajakutana katika mechi ya kirafiki au ya mashindano hivyo itakuwa kipimo tosha