BUNDI AENDELEA KULIA MSIMBAZI, HASSAN KESSY ATUPIWA VIRAGO, BANDA NAYE ASUSA
Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM
BAADA ya juzi kutangaza kujitoa kwenye kikosi cha Simba, beki Hassan Ramadhan Kessy ametupiwa virago vyake na uongozi wa Simba leo huku beki mwenzake wa kati Abdi Banda akijifukuzisha mwenyewe.
Kamati ya utendaji ya Simba iliketi leo makao makuu ya klabu mtaa wavMsimbazi ambapo ilipitia suala la Kessy na kuona mchezaji huyo alimfanyia rafu mbaya ya makusudi mshambuliaji wa Toto Africans Edward Christopher na kupewa kadi nyekundubiliyoigharimu timu.
Kessy amekuwa mtovu wa nidhamu na hii ni mara ya pili, mara ya kwanza Kessy alijitoa kambini akishinikiza alipwe fedha zake wakati timu ikiwa katika maandalizi ya mchezo wa ligi msimu uliopita.
Hajji Manara ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Habari wa Simba amefafanua kuwa klabu ya Simba imemsimamisha Kessy kucheza mechi tano, ina maana Kessy atakosa mechi zote za msimu.
Naye kocha wa Simba Jackson Mayanja amewataka mashabiki wa Simba kutokata tamaa kwani bado wanayo nafasi ya kutwaa ubingwa, pia ameelezea kujiondoa kwa Abdi Banda kikosini, Mayanja amedai Banda amejiondoa mwenyewe Simba hasa baada ya kususa