NAFASI KWA YANGA USIKU HUU NA AL AHLY

Na Exipedito Mataruma,  ALEXANDRIA

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika Yanga Sc wanashuka uwanjani muda si mrefu leo hii kukwaruzana na Al Ahly ya Misri mchezo wa marudiano uwanja wa Borg Al Arab mjini Alexandria Misri.

Katika mchezo wa leo Yanga wanahitaji ushindi wa aina yoyote ama sare inayoanzia mabao 2-2 ili isonge mbele, Al Ahly wanahitaji sare isiyo na .mabao ili wavuke hatua ya makundi.

Timu hizo zilifungana mabao 1-1 mjini Dar es Salaam zilipokutana juma lililopita, kocha mkuu wa Yanga Mholanzi Hans Van der Pluijm ameelezea mchezo huo na kusema vijana wake wana kila sababu ya kuibuka na ushindi.

Nahodha wa Yanga Nadir Haroub maarufu Cannavaro amewatoa wasiwasi wapenzi wa Yanga na Watanzania kwa ujumla kuwa ni lazima wapate ushindi hii leo

Wachezaji wa Yanga wakishangilia ushindi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA