MICHANO: PHILIPO NYANDINDI "O TEN", ALISAHAU MSEMO HUU, UKIMUONA KOBE JUU YA MTI UJUE KAWEKWA

Na Mkola Man, TANGA

YAP....yap....yap Michano yangu ya leo inamchana Philipo Nyandindi "O Ten" kutoka mji kasoro bahari yaani Morogoro ila safari yake kimuziki ilianzia Upanga jijini Dar es Salaam katika kundi la East Coast Team.

Lakini kabla hajatua kundi hilo, O Ten alikuwa msanii wa kujitegemea huko Morogoro na siku moja wakati msanii Inspekta Haroun akitamba na 'Mtoto wa geti kali' alivutiwa na msanii huyo jukwaani na kuamua kumleta Dar es Salaam.

Inspekta ndiyo msanii wa kwanza kurekodi studio na O Ten wimbo unaojulikana kwa jina la "Siku za Hukumu ya mwisho'. na hapo ndipo safari ya O Ten ilipoanza.

KWANINI ALIINGIA EAST COAST

O Ten alijiunga na East Coast Team baada ya kutelekezwa na Inspekta ambaye alimuahidi kumsaidia kimuziki ndipo alipotua kundi hilo lililotamba sana, mwaka 2004 alitoka na nyimbo iitwayo 'Nicheki' iliyotengenezwa vizuri na prodyuza P Funk Majani iliyompa heshima ndani ya kundi lake na nje pia.

Kisha nyota yake ikaanza kung' ara na akajipatia mashabiki wengi na kuweka historia ya kufanya shoo na wapinzani wao TMK Wanaume Family katika ukumbi wa Bilicanas, kundi la East Coast lina wasanii maarufu kama King Crazy GK, Mwana FA, Pouline Zongo, Snare, Buff G, AY na O Ten mwenyewe.

Chakusikitisha sana kabla ajapata mafanikio akaanza malumbano na msanii mwenzake Afande Sele ambaye anatoka naye Morogoro akichukua muda mrefu East Coast Team ikavunjika na hapo ndipo ukawa mwisho wake licha kwamba alikongoja kidogo kwa kutoa wimbo "Akipendacho binti".

O Ten alisahau maneno ya waswahili ambayo yalitimia yanayosema ukimkuta kobe juu ya mti usishangae ujue amepandishwa, na O Ten hakuonekana tena mpaka leo, Yap Mkola Man naachia line, tukutane Ijumaa ijayo

Philipo Nyandindi "O Ten"

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA