MITANANGE MIWILI FA CUP KUPIGWA LEO, NANI KUCHEZA FAINALI

Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM

MICHUANO ya Azam Sports Federation Cup inatarajia kuendelea jioni ya leo katika viwanja viwili tofauti hatua ya Nusu fainali ambapo timu mbili zitafuzu fainali itakayopigwa mwezi Mei mwaka huu.

Tukianzia pambano linalosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka katika miji ya Dar es Salaam na Tanga, mabingwa watetezi wa ligi kuu bara Yanga Sc watakuwa wageni wa Coastal Union ya Tanga uwanja wa CCM Mkwakwani.

Timu hizo zinakutana leo katika michuano hiyo inayofahamika zaidi kama FA Cup, Yanga inataka kulipiza kisasi kwani ilibutuliwa mabao 2-0 na vijana hao wa Wana Mangushi, Yanga ilifungwa kwenye mchezo huo wa ligi kuu bara.

Hivyo mchezo huo utakuwa mkali ikitaka kulipiza kisasi, pia ina machungu ya kutolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao 3-2 na Al Ahly ya Misri, Coastal nao kwa sasa wako vizuri hasa baada ya kupata ushindi wa mara mbili mfululizo.

Coastal iliifunga Simba Sc mabao 2-1 mchezo wa Robo fainali ya FA Cup, pia ikaifunga JKT Ruvu bao 1-0 mchezo wa ligi kuu bara hivyo leo inataka kuendeleza ubabe kwa Yanga, tusubiri nini kitatokea.

Mjini Shinyanga katika uwanja wa Mwadui Complex, wenyeji Mwadui Fc itaialika Azam Fc ambao ni klabu bingwa Afrika mashariki, timu hizo zimekamiana vya kutosha katika Nusu fainali hiyo nyingine.

Kocha wa Mwadui Fc Jamhuri Kihwelu "Julio" amejitamba kumbwaga mzungu wa Azam Stewart Hall raia wa Uingereza, Azam nayo kama Yanga ina hasira ya kutolewa kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika, Azam ilifungwa jumla ya mabao 4-2 na Esperance ya Tunisia.

Mwadui nao wana kumbukumbu mbaya ya kupoteza mechi mbili mfululizo za ligi kuu bara hivyo mchezo wa leo utakuwa mgumu na wakusisimua

Yanga Sc je watalipa kisasi?

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA