SIMBA KAZI MOJA TU, YAPIGA MAZOEZI YA HATARI, AZAM KAZI MNAYO
Na Salum Fikiri Jr, ZANZIBAR
KLABU ya Simba imejichimbia Zanzibar wakiweka kambj kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu bara na Azam Fc uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Vijana wa Simba wameendelea na mazoezi makali chini ya kocha wake Jackson Mayanja raia wa Uganda ambayo yanawafanya wachezaji wa Simba kuwa fiti zaidi.
Simba inacheza na Azam Fc Mei Mosi mwaka huu mchezo utakaotoa majibu nani anaweza kugombania ubingwa wa bara, Simba inakamata nafasi ya pili nyuma ya Yanga ikiwa na pointi 57 mechi 25, wakati Azam inashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 55 mechi 24